13258841_1713378792244504_924629682_n
Msanii wa Hip Hop Bongo, Bill Nas amefunguka kuhusiana na tetesi za kuhusishwa kujiunga na lebo ya WCB.

Akiongea na kipindi cha Clouds E cha Clouds TV, rapper huyo amesema kuwa taarifa hizo si za kweli.
“WCB ni lebo kubwa kwa sasa Afrika Mashariki nadhani hilo lipo wazi kabisa ila suala la mimi kwenda Wasafi aisee hata mwenyewe nimeshangaa, maana hata sijawahi kuongea na uongozi wa WCB wala sijawahi kwenda hata studio kwao, naona limekuwa kubwa hadi washkaji zangu wananipigia simu wakiniulizia lakini si kweli kabisa hilo suala,” alisema Bill Nas.
Kwa sasa Bill anafanya vizuri na ngoma yake Chafu Pozi.

BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


Je wewe una mtaji wa Ths.250,000/= au 510,000 au 1,020,000?..na unahitaji kufanya biashara kubwa kwa mtaji huo ufanikiwe?..basi kama ndiyo njoo tukuonyesha njia ya kutekeleza malengo yako...piga 0625 539 100

 
Top