Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) anayetambulika na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Profesa Ibrahim Lipumba, leo anatarajiwa kuanza ziara katika mikoa mbalimbali.

Katika ziara hiyo Profesa Lipumba ataandamana na viongozi watano waliosimamishwa uanachama na Baraza Kuu la Uongozi, ambapo pamoja na mambo mengine atafanya vikao vya ndani na wanachama na viongozi wa ngazi za wilaya kueleza kiini cha mgogoro uliopo ndani ya CUF.

Profesa Lipumba atafanya ziara hiyo katika mikoa mitatu ya Lindi, Mtwara na Tanga huku Jumuiya ya Vijana ya chama hicho, (JUVICUF), ikiwataka wanachama na viongozi kutompa ushirikiano kiongozi huyo.

Kambaya afafanua

Akizungumza jana, Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhuano wa Umma, ambaye amesimamishwa uanachama, Abdul Kambaya, alisema ziara ya Profesa Lipumba mikoani imetokana na mwaliko alioupata kutoka kwa wanachama na wananchi wa mikoa ya kusini.

Alisema kitendo cha mwenyekiti wa Vijana wa JUVICUF kuzuia wananchi wasimpatie ushirikiano Profesa Lipumba  ni sawa na kulewa madaraka ya ujana kwani hana mamlaka hayo.

“Sisi hatubabaishwi na Bobali lazima tutafanya ziara kesho (leo)  kwa sababu yeye si msemaji wa wilaya na hii ziara Perofesa Lipumba amepewa mwaliko na viongozi na wanachama wa CUF,” 
alisema Kambaya.

Wakati huohuo upande wa uongozi wa CUF ambao unamuunga mkono Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, umesema unashangazwa  na kitendo cha Profesa Lipumba kufungua akaunti mpya ya chama kupitia Benki ya NMB tawi la Ilala.

BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


Je wewe una mtaji wa Ths.250,000/= au 510,000 au 1,020,000?..na unahitaji kufanya biashara kubwa kwa mtaji huo ufanikiwe?..basi kama ndiyo njoo tukuonyesha njia ya kutekeleza malengo yako...piga 0625 539 100

 
Top