MSAJILI WA MAHAKAMA KUU AJITOA KWENYE KESI YA BABU TALE | Masama Blog


MSAJILI WA MAHAKAMA KUU AJITOA KWENYE KESI YA BABU TALE

Babu TALE
Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Projest Kahyoza amejitoa kusikiliza shauri linalowakabili
wakurugenzi wa kampuni ya Tiptop Connections ya jijini Dar es Salaam, Hamis Shaaban maarufu Babu Tale na ndugu yake, Idd Shaaban.
Kahyoza alifikia uamuzi huo juzi, siku aliyopanga kutoa maelekezo maalumu kwa wadaiwa hao. Hata hivyo, mlalamikaji Sheikh Hashim Mbonde alimuomba ajitoe kwa madai kuwa hana imani naye.
Katika shauri hilo, Babu Tale na nduguye wanatakiwa kujieleza ni kwa nini wasifungwe jela kwa kushindwa kutekeleza amri ya Mahakama hiyo.
Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam ilimtaka Babu Tale amlipe Shekh Hamis Mbonde, shilingi milioni 250 kwa kudaiwa kuvunja mkataba kati yake na Sheikh Mbonde wa kuuza na kusambaza nakala za mawaidha (DVDs) bila ridhaa ya sheikh huyo.
Source:Mwananchi

BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


UNAIJUA BIASHARA YA FOREVER LIVING?....Kama una mtaji kuanzia 250,000 hadi 1,020,000 na unapenda kujikwamua na kubadilisha maisha yako kupitia biashara hii Tupigie simu nambari 0625539100 au 0625539200