Hii ndiyo Kauli ya BMT kuhusu Yanga kukodishwa kwa miaka 10 | Masama Blog


Hii ndiyo Kauli ya BMT kuhusu Yanga kukodishwa kwa miaka 10

Baraza la michezo Tanzania BMT leo October 7 2016 limetangaza msimamo wake ikiwa ni siku moja imepita toka klabu ya Dar es Salaam Young Africans iweke wazi mkataba wake wa kukodiwa na kampuni ya Yanga Yetu Limited, Yanga ilitangaza jana October 6 mkataba walioingia na Yanga Yetu Limited Septemba 2016.
Baraza la michezo leo limetangaza kutoutambua mkataba huo wa Yanga ambao Yanga Yetu Limited waliingia na klabu ya Yanga kupitia kwa bodi ya wadhamini wa Yanga, katibu mkuu wa BMT Mohamed Kiganja amesema kuwa bodi ya wadhamini wa Yanga ni ya mpito na sio sawa kufanya maamuzi ya kuikodisha timu.
“Hivi karibuni kulikuwa na sakata kubwa kwa vilabu vyetu vya Simba na Yanga sijui kukodishwa sijui kuuzwa, sisi kama baraza tunajua watu wanaofanya hivi wana yao moyoni wameona kama uendeshwa wa michezo wa sasa hivi unaleta matatizo, baraza lina bariki mabadiliko lakini yafuate utaratibu”

BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


UNAIJUA BIASHARA YA FOREVER LIVING?....Kama una mtaji kuanzia 250,000 hadi 1,020,000 na unapenda kujikwamua na kubadilisha maisha yako kupitia biashara hii Tupigie simu nambari 0625539100 au 0625539200