Diamond Platnumz a.k.a Mzee wakusema nawe azua taflan baada ya kumlipua X GIRL FRIEND wake Wema Sepetu sasa mambo hadharani

BAADA ya muigizaji nyota Wema Sepetu ‘kumtusi’ mpenziwe wa zamani, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, kwa kudhihaki zawadi ya bei chee ya gari aliyowahi kumnunulia, rais huyo wa lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), juzikati aliibuka na kumjibu kuwa amefanya mambo ya 
‘Kiswahili’.
Akizungumza ofisini kwake Sinza Mori jijini Dar es Salaam, Diamond alisema katika maisha kila mmoja ana ndoto zake, hivyo ni jambo jema kwamba amefanikisha, lakini hata hivyo, akasema hatua aliyofikia yeye siyo ya kufanya mashindano na mtu, badala yake ni kuchapa kazi kusaka mafanikio zaidi ya maisha yake.
“Kiukweli kabisa nampongeza Wema kwa kununua gari maana hiyo ndiyo ilikuwa mipango ya maisha yake, maneno anayosema kwamba mimi nilimnunulia gari la elfu thelathini ndipo nilipomuona wa ajabu. Sikuona umuhimu wa kunizungumzia pale.
“Hayo ndiyo mambo ya Kiswahili. Mimi siyo mtu wa kushindana kununua gari tena, maana hatua hiyo tayari nimeshapita, zaidi nawaza kupiga kazi na kujitengenezea maisha yangu mapya yatakayoweza kuifanya familia yangu iishi kwa raha na amani kipindi chote cha uhai wangu, najua kuna watu bado wanafikiria mimi ni limbukeni wa vitu kama zamani, kwa sasa sifikirii mashindano, ninaangalia kazi zinazoweza kuniingizia kipato tu,” alisema Diamond.
Katika pati aliyoiandaa hivi karibuni kusherehekea siku yake ya kuzaliwa, Wema pamoja na mambo mengine, aliwaonyesha waalikwa zawadi ya gari aina ya Range Rover aliyojinunulia, akitoa maneno yaliyoonyesha kumponda Diamond, kwamba ameinunua kwa kiasi cha dola za Marekani 90,000 (karibu shilingi milioni 200 za Kitanzania), tofauti na watu wanaojikweza kwa ‘vigari vyao vya elfu thelathini’


Kujua Mbinu Za Kumfikisha Kileleni Mwanamke Kwa Haraka: BONYZA HPA CHNI

Kujua Sehemu 10 Zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, BONYZA HAP 1UU
BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
© Copyright Masama Blog | Designed By MASAMA TEAM
Back To Top