CHADEMA yapinga kununuliwa na Lowassa, yashindwa kuzungumzia tuhuma za ufisadi.Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema ni uongo na ni propaganda za wapinzani wao kwamba Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa alimhonga Mwenyekiti Freeman Mbowe ili kupata nafasi ya kugombea urais mwaka 2015.

Dkt.  Mashinji ameyasema hayo katika kipindi cha Kikaangoni  kinachorushwa na kituo cha EATV kupitia ukurasa wa facebook ambapo wananchi walikuwa wakimuuliza maswali ya papo kwa papo naye anayajibu.

“Si kweli kwamba Mwenyekiti Freeman Mbowe alimhonga Lowassa ili agombee urais kupitia CHADEMA , ni propaganda zinazoenezwa na wapinzani wetu ili kuwadanganya wananchi” Amesema Dkt. Mashinji.

Amesema Lowassa alijiunga na CHADEMA kwa njia halali kwa mujibu wa taratibu za chama, na maamuzi ya kumteua kugombea urais yalifanywa na vikao halali kuanzia ngazi ya Kamati Kuu hadi Mkutano Mkuu.

Kuhusu sababu za CHADEMA kumkaribisha Lowassa licha ya kumtaja miaka mingi kuwa alihusika na ufisadi, Dkt Mashinji, hakutaka kulifafanua kwa undani, lakini aliishia kusema kuwa wao walijiridhisha kuwa hakuwa na hatia yoyote na kwamba kama kweli alikuwa ni fisadi, basi vyombo vya dola vingemchukulia hatua.

"Kama mtu kweli alikuwa ni fisadi, kwanini hakuwahi kuchukuliwa hatua, hata kufikishwa mahakamani?, nadhani hilo tuliache" Alisema kwa ufupi Dkt Mashinji.

Aidha Dkt. Mashinji amewataka watanzania na wapenzi wa CHADEMA kufahamu kwamba chama hicho hakipo kimya bali kinaendelea na mikakati ya kuhakikisha kwamba kinawafikia watanzania kwa kuwatetea kwa kila hali kutokana na mambo yanayoendelea nchini.

Kujua Mbinu Za Kumfikisha Kileleni Mwanamke Kwa Haraka: BONYZA HPA CHNI

Kujua Sehemu 10 Zinazompa Raha mwanamke wakati wa Tendo, BONYZA HAP 1UU
BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip.
© Copyright Masama Blog | Designed By MASAMA TEAM
Back To Top