BREAKING NEWZZZ…BONDIA THOMAS MASHALI AUWAWA USIKU WA KUAMKIA LEO..SOMA ZAIDI HAPA | Masama Blog


BREAKING NEWZZZ…BONDIA THOMAS MASHALI AUWAWA USIKU WA KUAMKIA LEO..SOMA ZAIDI HAPA

Bondia Thomas Mashari ameuawa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo.
BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini Thomas Mashali ‘Simba asiyefugika’ ameuawa usiku wa kuamkia leo na watu wasiojulikana na mwili wake umeokotwa maeneo ya Kimara kabla ya kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Rais wa Oganizesheni ya Ngumi za kulipwa (TPBO) Yassini Abdallah ‘Ustadh’ alisema mauti yalimkuta bondia huyo baada ya kupigwa na watu wasiojulikana na mwili wake kuokotwa na wasamalia wema maeneo ya Kimara.
“Ni kweli Mashali amefariki dunia nimepokea Habari hiyo muda mfupi uliopita sasa nipo njiani naelekea Muhimbili” alisema Ustadhi.
Taarifa za utaratibu wa mazishi zitatolewa baadae na ndugu wa marehemu.

BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


UNAIJUA BIASHARA YA FOREVER LIVING?....Kama una mtaji kuanzia 250,000 hadi 1,020,000 na unapenda kujikwamua na kubadilisha maisha yako kupitia biashara hii Tupigie simu nambari 0625539100 au 0625539200