Azam FC imemtambulisha Abdul Mohamed aliyekuwa BBC | Masama Blog


Azam FC imemtambulisha Abdul Mohamed aliyekuwa BBC

Mabingwa wa Afrika Mashariki na kati klabu ya Azam FC leo October 6 2016 imetangaza rasmi kuongeza nguvu katika safu ya uongozi wa klabu hiyo, Azam FC ambao wanashiriki Ligi Kuu Tanzania bara na wapo nafasi ya 6 katika msimamo wa Ligi hiyo wamemtambulisha meneja mkuu wa klabu hiyo
Kupitia kwa afisa mtendaji mkuu wa klabu hiyo Saad Kawemba ametangaza Azam FCkuingia mkataba na mtangazaji wa zamani wa Clouds na BBC Abdul Mohamed kama General Manager wa klabu hiyo, lengo wa likiwa ni kusaidiana majukumu sambamba lakini kwa kuzingatia weledi.
“Abdul Mohamed ni mwenzetu tunamtambulsha rasmi kabisa kuwa ni mwenzetu ameingia katika familia ya Azam FC takribani mwezi mmoja uliopita, tupo nae anaingia katika sekretarieti ya Azam FC kama general manager” >>> Saad Kawemba

BOFYA LIKE KUUNGANA NASI FACEBOOK!


UNAIJUA BIASHARA YA FOREVER LIVING?....Kama una mtaji kuanzia 250,000 hadi 1,020,000 na unapenda kujikwamua na kubadilisha maisha yako kupitia biashara hii Tupigie simu nambari 0625539100 au 0625539200