Ticker

10/recent/ticker-posts

HILI NDILO BALAA JIPYA LA MAKALIO YA KICHINA

mchina1
Tabia ya baadhi ya wasichana hasa wa mjini kuwa na tamaa ya kuwa na makalio makubwa na hivyo kulazimika kutumia dawa mbalimbali, imekuwa ikishamiri kila siku licha ya serikali kupiga marufuku uingizwaji wa dawa hizo
jayjay
jayjayJayjay

Gazeti hili matoleo yaliyopita liliwahi kuandika jinsi mastaa wengi Bongo wanavyotumia dawa hizo lakini uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa, kasi ya matumizi ya dawa hizo yamekuwa yakishamiri huku waathirika wengi wakijiuguza kwa siri baada ya kupata madhara.
gillaGilla.
Katika tukio jipya la hivi karibuni, mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Hamisa ambaye alidai ni mke wa mtu alisema kuwa, alishawishiwa na rafiki yake kutumia dawa hizo ili naye awe na ‘zigo’ lakini ameanza kuona zinamletea matatizo.
“Nimekuwa nikisikia kuwa dawa hizi zina madhara lakini kuna rafiki yangu mmoja ambaye aliwahi kutumia na yuko poa ndiye aliyenipeleka kwenye duka moja lililopo Kijitonyama na kununua. Awali sikuona tatizo lakini kadiri siku zinavyokwenda nahisi maumivu f’lani, najuta kuzitumia dawa hizi kwa kweli,” alisema mwanamke huyo. 
kidoa
kidoaKidoa.
OFM mtaani
Baada ya kupata malalamiko hayo, waandishi wetu walifanya uchunguzi na kubaini kuwa dawa hizo zinauzwa kwa siri sana tangu serikali icharuke na kutoa tamko la kuwashughulikia wale wanaoziuza.
Katika uchunguzi huo, yamegundulika maduka kibao mitaa ya Kariakoo, Kinondoni na Mwenge jijini Dar ambapo wauzaji huziuza dawa hizo ‘kimagutu’ kana kwamba wanauza madawa ya kulevya au bangi.

Mwandishi wetu alifika kwenye duka moja lililopo Msimbazi baada ya kulengeshwa kuwa dawa hizo zinauzwa hapo, muuzaji alipoulizwa uwepo wa dawa hizo, kwanza alikataa lakini baadaye alikubali huku akionekana ni mwenye wasiwasi.

Post a Comment

0 Comments