Ticker

10/recent/ticker-posts

Fahamu umuhimu wa kujua siku za hedhi.

MZUNGUKO WA HEDHI (WHEEL OF FORTUNE)


Katika mizunguko yangu ya kutoa ushauri wa afya kwenye mahusiano nimekutana na watu wengi ambao ninagundua ya kwamba hawajui kuhesabu siku zao za hedhi au hawajui mzunguko wao ni wa siku ngapi. Wanaume wengi ndio hawajui kabisa. Hivyo Health Point imeamua kuandika japo kidogo kuhusu uhesabuji wa siku za hedhi.

BAADHI YA SABABU ZINAZOPELEKEA WANAWAKE NA VIJANA WA LEO KUTOKUJUA KUHESABU SIKU ZAO ZA HEDHI.

1- Kupotea kwa elimu ya jando katika makabila yetu
2- Kupotea kwa elimu ya afya katika mashule na nyumba za kuabudia

3- Kuwa na familia za kisasa zisizojali maisha ya kiasili ya kifamilia na kujali zaidi maisha ya kisasa