Ticker

10/recent/ticker-posts

INAPOTOKEA UMEMPENDA MTU ALIYE NA MPENZI WAKE FANYA YAFUATAYO

Mapenzi yamekuwa yakichukua nafasi kubwa sana katika maisha yetu ya kila siku na yamekuwa yakichangia kwa kiasi kikubwa furaha kwa kila mtu. Kama huamini, angalia wale waliotokea kupenda na wao wakapendwa, utabaini nyuso zao zimetawaliwa na furaha isiyo na kifani. Lakini mapenzi hayo hayo yamekuwa ni chanzo cha vilio kwa baadhi ya watu. Mpenzi msomaji wangu, kupenda hakuna macho! Moyo ukishapenda hausikii la kuambiwa. Katika hili ndiyo maana unaweza kumuona mwanaume kazimika kwa demu ambaye hawaendani kabisa lakini moyo wake ndiyo umeshapenda. Ilishawahi kutokea msichana akampenda kijana mmoja ambaye ni fukara kupita maelezo. Yeye akawa ndiyo anamhudumia kwa kila kitu. Akamfanyia mpango wa ajira na mwisho wake wakafunga ndoa. Sasa hivi wanaishi maisha ya furaha na amani. Wamegeuka mfano wa kuigwa kwa jinsi wanavyopendana lakini huko nyuma msichana huyo alikuwa akichekwa kwa kutoa penzi kwa mwanaume asiye na mbele wala nyuma. Hayo ndiyo mapenzi jamani! Lakini pia katika kufurukuta kumtafuta mpenzi wa kuwa naye maishani, mwanaume anaweza kujikuta unaangukia kwa demu ambaye tayari ana mpenzi wake.  Moyo wako unakuambia yeye ndiye mtu sahihi katika maisha yako lakini tayari ana mtu wake, unafanyaje?  Utapambana kuhakikisha unapata kile ambacho moyo wako umekipenda au utakubaliana na ukweli kwamba huwezi kuwa naye kwa kuwa ana mtu wake? Inapofikia hatua hiyo unaweza kujikuta upo njia panda hasa pale ambapo huyo mwenye mtu wake naye anaonesha kuwa na chembechembe za mapenzi kwako. Kuna mambo kadhaa ya kukusaidia kukabiliana na hali hii. Chunguza Tumia muda wako mwingi kuchunguza juu ya uhusiano wake. Uhusiano wao umesimama na wanaonekana ni watu wenye ‘future’? Nasema hivyo kwa sababu, yawezekana uhusiano wa huyo uliyetokea kumpenda ni wa kuzuga tu na huenda wewe ndiye mwenye ‘future’ naye. Ndiyo maana nikasema chunguza uhusiano wake kwanza. Usitafute uadui Baada ya kuchunguza, ukibaini kwamba uhusiano wao hauko ‘siriasi’, vuta subira, lolote linaweza kutokea na likaufurahisha moyo wako. Lakini kama utaona ni watu walio siriasi na wanaelekea kuoana, usitafute uadui bure, kaa pembeni. Una nafasi kwake? Sawa umetokea kumpenda msichana aliye na mtu wake, umeshawahi kujiuliza kama una nafasi ndani ya moyo wake? Anaonesha dalili fulani za kukupenda kama unavyompenda na ni mtu anayeonesha kukumisi anapokuwa mbali na wewe? Utakapobaini una nafasi kwake, uamuzi wa kumpotezea hautakuwa na nafasi. Ni rahisi kubadili uamuzi wake? Unadhani huyo uliyetokea kumpenda anaweza kubadili maamuzi ya kumuacha huyo aliyenaye kama kweli hawana ‘future’? Utagundua hilo kwa kuongea naye na kumsikia kama anaweza kufanya maamuzi hayo ili awe na wewe. Pingana na moyo wako Ifike wakati upingane na moyo wako. Unajua moyo wako kukuambia kuwa unataka kuwa na uhusiano na demu ambaye tayari ana mpenzi wake wakati mwingine utakuwa unakupotosha.  Kwa hiyo ukiona vipi, pingana nao. Acha kumng’ang’ania msichana mwenye mpenzi wake licha ya ukweli kwamba, huenda wewe ndiye mwenye nafasi ya kuwa mume wake na siyo huyo aliye naye. Urafiki ni poa? Umempenda sana na hauko tayari kumkosa katika maisha yako lakini imetokea kwamba tayari yuko na mtu na umebaini huna nafasi kwake kabisa? Usiumie, omba angalau urafiki. Siyo urafiki wa kivile sana ila angalau pale unapotaka kusikia sauti yake kwa kumsalimia tu, upate nafasi hiyo. Usiumie, yupo mwingine Haina haja ya kujitafutia vidonda vya tumbo bure kwa kuwa tu umebaini uliyetokea kumpenda tayari ana mtu. Chukulia ni hali ya kawaida, mademu wazuri ambao wanaishi singo wapo kibao huko mtaani, ni suala la wewe kutulia tu. Amini yupo mwingine ambaye atayafanya maisha yako yawe ya furaha. Naomba nihitimishe kwa kusema kwamba, unapotokea kumpenda mtu fulani, pambana kuhakikisha unampata kwa sababu ukimkosa maisha yako yanaweza kuwa gizani. Ila pale utakapoona uwezekano wa kuwa naye haupo, usilazimishe ndugu yangu. Kumbuka haya ni maisha tu!    Mambo ya kuzingatia unapomtumia mpenzi wako zawadi Nazungumzia ishu ya wapenzi kununuliana zawadi. Hapa sizungumzii zawadi ambazo wengi wetu tumekuwa tukinunuliana siku za Sikukuu kama vile Iddi, Krismasi, Valentine na nyinginezo bali namaanisha zawadi nje ya siku hizo. Kumtumia mwenzi wako zawadi ni kati ya mambo ambayo humfanya afurahie uhusiano wake na wewe. Hata hivyo, hakuna zawadi za moja kwa moja ambazo ni rasmi kwa ajili ya wapenzi lakini ni vyema ukamtumia zawadi kulingana na mapenzi yake zaidi. Kwa kuwa wewe unamfahamu zaidi mwenzi wako, unaweza kujua zawadi gani ni nzuri zaidi kwake au anayopendelea kuliko aina nyingine. Wiki hii nimechambua aina kuu za zawadi ambazo ukimtumia mpenzi wako utamteka hisia zake na ataona unamjali. Mavazi Mavazi ni kati ya zawadi ambazo zitamfanya mpenzi wako azidi kukupenda na kuwa karibu zaidi na wewe. Aina ya nguo ambazo unaweza kumtumia mpenzi wako ni zile ambazo unaamini atavutiwa nazo au zile ambazo zitampendeza na kumfanya aonekane nadhifu.Hata hivyo, zipo aina za mavazi ambazo zimependekezwa zaidi kwa ajili ya wenzi kutumiana wanapokuwa mbali na hata wanapokuwa karibu. Kama wewe ni mwanamke unataka kumtumia mpenzi wako wa kiume, mavazi yafuatayo yanafaa zaidi. Saa nzuri ya mkononi, nguo za ndani, lakini lazima uzingatie rangi ya bluu, bluu bahari au nyeupe kimsingi zisiwe za rangi zinazoficha uchafu. Zingine ni fulana za ndani ‘singlendi’, fulana, mkanda wa suruali, simu ya mkononi, vitambaa vya jasho n.k. Hakikisha katika zawadi hizo, unaambatanisha na manukato mazuri hasa yale ambayo unajua atayapenda. Haishauriwi kumtumia suruali au shati kwa sababu inaweza kuwa kubwa au ndogo, hivyo kupunguza ladha ya zawadi hasa kama atakuwa ameipenda sana. Zawadi za aina hiyo, unaweza kumpa mwenzi wako ofa ya kwenda kuchagua moja kwa moja dukani lakini kama unajua saizi yake na una uhakika akivaa atapendeza, ruksa kumnunulia vitu hivyo na tena utakapopatia saizi yake vizuri ataamini uko makini naye na unampenda kwa dhati. Kama wewe ni mwanaume na unataka kumtumia mpenzi wako wa kike zawadi, lazima uwe makini sana! Mavazi yaliyopendekezwa hapa ni pamoja na batiki (gauni, blauzi na sketi, blauzi yenyewe n.k), hereni, bangili, mkufu, simu ya mkononi, saa ya mkononi, nguo za ndani (kulingana na mapendekezo yake, kwa jinsi umjuavyo), sidiria, viatu n.k. Kama umesoma vizuri utaona mwanamke anaweza kununuliwa vitu vingi zaidi (hasa nguo) tofauti na mwanaume. Hii inatokana na aina za mavazi na saizi zao kukaririka kirahisi zaidi au kutokuwa na saizi ya moja kwa moja. Mathalan, batiki, sketi na blauzi na vinginevyo. Kama kawaida, mavazi haya, ambatanisha na manukato mazuri, hasa yale ambayo ndiyo anayopendelea mpenzi wako. Maua pia ni kati ya zawadi zinazopendekezwa na wataalamu wa mambo ya mapenzi. Maua ni mazuri sana kwa mwezi aliye mbali, lakini ni vyema kuzingatia na umbali uliopo kati yenu, kwani maua huweza kusinyaa kabla ya kumfikia (hasa kama ukimtumia yale halisi, kwani ndiyo haswa mazuri). Hata hivyo, zipo zawadi nyingine ambazo unaweza kumtumia mpenzi wako kwa kuangalia vitu anavyovipenda sana. Hii ni njia pekee ya kuonesha ubunifu wako na jinsi unavyomjali hata akiwa mbali kwa kumtumia vitu ambavyo huwa anavipenda lakini alipo hawezi kuvipata! Mathalan, mpenzi wako anapenda sana zabibu lakini amekwenda mkoa ambao vitu hivyo havipatikani kwa urahisi, hii ni nafasi yako kumtumia. Mathalan unajua kabisa anapenda sana kusoma vitabu lakini sehemu aliyopo hawezi kupata, basi nunua majarida, magazeti na matoleo yote ambayo hajayapata kisha mtumie, hakika utakuwa umemfurahisha sana na kumfanya afurahi kupata vitu hivyo. Kwa leo naomba niishie hapo, lengo ni kukufahamisha kwamba zawadi ni kitu muhimu sana katika kuliboresha penzi lenu. Kwanza mpenzi wako aamini kwamba unampenda lakini pia unamjali. Nazungumzia ishu ya wapenzi kununuliana zawadi. Hapa sizungumzii zawadi ambazo wengi wetu tumekuwa tukinunuliana siku za Sikukuu kama vile Iddi, Krismasi, Valentine na nyinginezo bali namaanisha zawadi nje ya siku hizo. Kumtumia mwenzi wako zawadi ni kati ya mambo ambayo humfanya afurahie uhusiano wake na wewe. Hata hivyo, hakuna zawadi za moja kwa moja ambazo ni rasmi kwa ajili ya wapenzi lakini ni vyema ukamtumia zawadi kulingana na mapenzi yake zaidi. Kwa kuwa wewe unamfahamu zaidi mwenzi wako, unaweza kujua zawadi gani ni nzuri zaidi kwake au anayopendelea kuliko aina nyingine. Wiki hii nimechambua aina kuu za zawadi ambazo ukimtumia mpenzi wako utamteka hisia zake na ataona unamjali. Mavazi Mavazi ni kati ya zawadi ambazo zitamfanya mpenzi wako azidi kukupenda na kuwa karibu zaidi na wewe.  Aina ya nguo ambazo unaweza kumtumia mpenzi wako ni zile ambazo unaamini atavutiwa nazo au zile ambazo zitampendeza na kumfanya aonekane nadhifu.Hata hivyo, zipo aina za mavazi ambazo zimependekezwa zaidi kwa ajili ya wenzi kutumiana wanapokuwa mbali na hata wanapokuwa karibu. Kama wewe ni mwanamke unataka kumtumia mpenzi wako wa kiume, mavazi yafuatayo yanafaa zaidi. Saa nzuri ya mkononi, nguo za ndani, lakini lazima uzingatie rangi ya bluu, bluu bahari au nyeupe kimsingi zisiwe za rangi zinazoficha uchafu.  Zingine ni fulana za ndani ‘singlendi’, fulana, mkanda wa suruali, simu ya mkononi, vitambaa vya jasho n.k. Hakikisha katika zawadi hizo, unaambatanisha na manukato mazuri hasa yale ambayo unajua atayapenda. Haishauriwi kumtumia suruali au shati kwa sababu inaweza kuwa kubwa au ndogo, hivyo kupunguza ladha ya zawadi hasa kama atakuwa ameipenda sana. Zawadi za aina hiyo, unaweza kumpa mwenzi wako ofa ya kwenda kuchagua moja kwa moja dukani lakini kama unajua saizi yake na una uhakika akivaa atapendeza, ruksa kumnunulia vitu hivyo na tena utakapopatia saizi yake vizuri ataamini uko makini naye na unampenda kwa dhati. Kama wewe ni mwanaume na unataka kumtumia mpenzi wako wa kike zawadi, lazima uwe makini sana! Mavazi yaliyopendekezwa hapa ni pamoja na batiki (gauni, blauzi na sketi, blauzi yenyewe n.k), hereni, bangili, mkufu, simu ya mkononi, saa ya mkononi, nguo za ndani (kulingana na mapendekezo yake, kwa jinsi umjuavyo), sidiria, viatu n.k. Kama umesoma vizuri utaona mwanamke anaweza kununuliwa vitu vingi zaidi (hasa nguo) tofauti na mwanaume. Hii inatokana na aina za mavazi na saizi zao kukaririka kirahisi zaidi au kutokuwa na saizi ya moja kwa moja. Mathalan, batiki, sketi na blauzi na vinginevyo. Kama kawaida, mavazi haya, ambatanisha na manukato mazuri, hasa yale ambayo ndiyo anayopendelea mpenzi wako. Maua pia ni kati ya zawadi zinazopendekezwa na wataalamu wa mambo ya mapenzi. Maua ni mazuri sana kwa mwezi aliye mbali, lakini ni vyema kuzingatia na umbali uliopo kati yenu, kwani maua huweza kusinyaa kabla ya kumfikia (hasa kama ukimtumia yale halisi, kwani ndiyo haswa mazuri). Hata hivyo, zipo zawadi nyingine ambazo unaweza kumtumia mpenzi wako kwa kuangalia vitu anavyovipenda sana. Hii ni njia pekee ya kuonesha ubunifu wako na jinsi unavyomjali hata akiwa mbali kwa kumtumia vitu ambavyo huwa anavipenda lakini alipo hawezi kuvipata!  Mathalan, mpenzi wako anapenda sana zabibu lakini amekwenda mkoa ambao vitu hivyo havipatikani kwa urahisi, hii ni nafasi yako kumtumia. Mathalan unajua kabisa anapenda sana kusoma vitabu lakini sehemu aliyopo hawezi kupata, basi nunua majarida, magazeti na matoleo yote ambayo hajayapata kisha mtumie, hakika utakuwa umemfurahisha sana na kumfanya afurahi kupata vitu hivyo.  Kwa leo naomba niishie hapo, lengo ni kukufahamisha kwamba zawadi ni kitu muhimu sana katika kuliboresha penzi lenu. Kwanza mpenzi wako aamini kwamba unampenda lakini pia unamjali