Ticker

10/recent/ticker-posts

WASANII BABY MADAHA NA INSPECTOR WANASWA WAKIFANYA YAO BILA HIYANA!..CHEKI HAPAA

 
Staa wa Bongo Fleva, Haroun Kahena ‘Inspector Haroun’ akigonga busu shavuni kwa Baby Madaha. Tukio hilo lilinaswa na kamera ya paparazi wetu hivi karibuni kwenye pub moja iliyopo maeneo ya Kijitonyama jijini Dar ambapo awali Inspector alionekana akiwa amemkalia Madaha huku wakipigana mabusu. Baada ya paparazi wetu kujitokeza na kuanza kuwafotoa, Inspector ambaye ni mume wa mtu alishituka na kujinasua kutoka kwenye mwili wa mwanadada huyo.Katika hali ya kushangaza, mastaa wawili wa muziki, Baby Madaha na Haroun Kahena ‘Inspector Haroun’ wamenaswa usiku wakila bata huku wakiwa kimahaba.
 
Mtu mzima ‘Inspector Haroun’ na Baby Madaha wakizuga flani hivi... baada ya kuhisi uwepo wa paparazi wetu eneo la tukio.
Alipoulizwa juu ya kile alichokuwa akifanya wakati ni mume wa mtu, Inspector alisema: “Kaka kwani kuna kibaya gani tulichokuwa tunafanya, tupo hapa tunapanga mambo yetu ya muziki na wala hakuna ishu zaidi.”
 
Kwa pamoja wawili hao wakipozi kimahaba. Baby Madaha kwa sasa haijulikani anatoka kimapenzi na nani ila Inspector Haroun ni mume wa Bahati ambaye alifunga naye ndoa mwaka 2004 na wamejaaliwa kupata watoto wawili ambao ni Nassir na Shadya.